Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeondoka kwenda Morocco kwa mchezo wa kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Madagascar utakaochezwa Septemba 29, 2026.
Stars inauendea mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Equatoria Guinea kwa mabao 2-0.
Mara ya mwisho ya Stars kukutana na Madagascar inakumbukumbu ya kushinda kwa mabao 2-1 kwenye mashindano ya CHAN mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 9, 2025, mabao ya Stars yakifungwa Clement Mzize ambaye kwa sasa hayupo kwenye kikosi hicho, huku bao la Madagascar likifungwa Mika Razafimahatana.