Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Simba Yaponzwa na Dabi Yapigwa Faini Mamilioni

Mchezo namba 077 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Dodoma Jiji FC dhidi ya Simba SC uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma mnamo Februari 25, 2026, ulimalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya 0-0.

Licha ya mashambulizi ya pande zote mbili, hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake katika mchezo huo wa mzunguko wa 10 wa ligi.

Hata hivyo, mchezo huo umeacha gumzo kufuatia mlolongo wa adhabu kali zilizotolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi dhidi ya wachezaji, viongozi, na klabu kwa ujumla:

• Adhabu kwa Klabu ya Simba: Klabu hiyo imetozwa faini ya Sh5 milioni kutokana na vitendo vya mashabiki wake kuwarushia chupa za maji mchezaji William Edgar wa Dodoma Jiji na watoa huduma ya kwanza (Red Cross) wakati wakitekeleza majukumu yao.

• Faini kwa Dodoma Jiji FC: Klabu ya Dodoma Jiji pia imetozwa faini ya Sh5 milioni baada ya maofisa wake na watoa huduma kuchelewa kuingia uwanjani kwa makusudi, kitendo kilichotafsiriwa kama hila ya kupoteza muda.

Mwamuzi Afungiwa Miezi Mitatu: Mwamuzi wa akiba (reserve referee), Charles Simon, amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kutafsiri sheria na kuruhusu Dodoma Jiji kufanya mabadiliko ya wachezaji mara nne (4) badala ya mara tatu (3) zinazoruhusiwa kikanuni.

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: