Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waamuzi Kombe la Dunia Wapigwa Marufuku Mechi za Kirafiki

Waamuzi Kombe la Dunia 2026 wapigwa marufuku mechi za kirafiki
Waamuzi walioteuliwa kuhudhuria mafunzo ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2026 yanayoendelea Doha, Qatar, wamepewa maelekezo mapya na thabiti kuelekea mashindano hayo.

Waamuzi hao wameagizwa kutoshiriki wala kuchezesha mechi zozote za kirafiki zinazohusisha timu ambazo zimefuzu na zitashiriki fainali hizo za mwaka 2026.

Hatua hiyo inalenga kulinda uadilifu na kuzuia upendeleo au malalamiko yoyote yanayoweza kujitokeza kabla ya kuanza kwa mashindano hayo makubwa katika nchi za Marekani, Canada, na Mexico.

Maagizo haya yanahakikisha kuwa waamuzi wanabaki bila upande wowote na wanazingatia viwango vya juu vya kitaaluma bila kuingiliana na timu shiriki mapema, huku wakijiandaa kwa mabadiliko mapya ya sheria yaliyoidhinishwa na Bodi ya Kimataifa ya Kandanda (IFAB)

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: