Kocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Miguel Gamondi amewaongeza wachezaji wawili kutoka Timu ya Taifa U17 (Serengeti Boys) Luqman Mbalasalu na Kassim Juma kwa mechi mbili za kirafiki kwenye kalenda ya FIFA. Wachezaji hao ambao wapo Morocco na Serengeti Boys watajiunga na kikosi hicho baada ya mechi ya fainali ya Mataifa ya Afrika (AFCON U17) dhidi ya Senegal itakayochezwa Juni 2, 2026.
Taifa Stars itacheza mechi ya kwanza na Uganda Juni 5, na ya pili didi ya Rwanda Juni 9, 2026 mjini Marrakech, Morocco. Wachezaji wengine wa Taifa Stars walioitwa kwenye kikosi hicho wataripoti kambini leo jijini Dar es Salaam.