Mvutano kati ya Richarlison na Tottenham Hotspur unaonekana kufikia hatua nyingine baada ya kocha Roberto De Zerbi kuweka wazi kuwa mshambuliaji huyo hatacheza, hata kwenye Carabao Cup.
De Zerbi amesisitiza kuwa kila upande unafahamu kilichotokea kati ya mchezaji na klabu, huku akiongeza kuwa Tottenham iliwahi kupoteza 3-0 dhidi ya Brentford ikiwa na Richarlison uwanjani.
Baada ya kauli hizo nzito, Richarlison alijibu kupitia akaunti yake ya X kwa emoji ya kulia 😢 — ishara inayoongeza zaidi sintofahamu kuhusu mustakabali wake Spurs.
Richarlison Kufungasha Virago?
- Chanzo:
- Clouds Media