Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewafungia waamuzi wawili wa mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Amaan kufuatia makosa ya kutafsiri sheria za mpira wa miguu.
Mwamuzi msaidizi namba moja Kassim Mpanga kutoka Dar es Salaam amefungiwa miezi sita baada ya kukataa bao halali la klabu ya Simba katika dakika ya 70 ya mchezo. Baada ya tathmini ya wataalamu wa sheria za mpira pamoja na uchambuzi wa video, ilibainika kuwa hakukuwa na kosa la kuotea kabla ya kufungwa kwa bao hilo.
Chanzo; Global Publishers