Baada ya tukio la Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA John Heche kuzuiwa na Idara ya Uhamiaji kuvuka mpaka wa Sirari ili kwenda Kenya, Idara hiyo imetoa taarifa usiku huu ikieleza yafuatayo.
Taarifa ya Idara hiyo imeeleza kuwa October 18, 2025 katika Kituo cha Uhamiaji cha mpaka wa Sirari Mkoani Mara, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, John Wegesa Heche ameondoka Nchini kwa kuvuka mpaka na kuingia Nchi jirani bila kufuata taratibu na kanuni za uhamiaji zilizoundwa chini ya sheria ya uhamiaji sura ya 54.
“Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa Raia wa Tanzania na Wageni wote wanaotoka na kuingia Nchini kufuata taratibu na kanuni zinazoongoza uingiaji, ukaazi na utokaji wa Watu nchini ili kuepuka kutenda kosa na kuchukuliwa hatua za kisheria” imeeleza taarifa hiyo.
Chanzo: Millard Ayo