Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mchakato Maombi Vitambulisho vya Taifa Waraisishwa

Mamlaka ya Vitambuisho vya Taifa (NIDA) imekuja na mfumo wa namba maalumu ambayo itatumiwa na wananchi kutuma ujumbe wa maandishi na kujibiwa wakati wa kutuma maombi ya kupata utambulisho wa taifa pamoja na kufuatilia taarifa mbalimbali, lengo likiwa ni kurahishisha zaidi mchakato wa huduma hiyo.

Kwa mujibu wa NIDA namba hiyo ni 15274 na kwamba wananchi wataitumia kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu bila malipo wakati wa kufuatilia maombi ya utambulisho, hatua za usajili pamoja na kujua kuwa vitambulisho vyao viko wapi ili waende kuchukua.

Akizungumza leo mkoani Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho NIDA, James Kaji, amesema kipindi cha nyuma kulikuwa na changamoto za kimifumo na hadi kusababisha wananchi kuwatuhumu watumishi wa NIDA, na kwamba yote yalikuwa yanasababishwa na mawasiliano.

"Ili kuondoa usumbufu kwa wananchi tumeamua kuja na namba ambayo itamsaidia mwananchi kujua hatua za usajili zinaendaje na kupata taarifa za kitambulisho au namba akiwa mahali kokote," amesema Kaji.

Alisema namba hiyo itamuwezesha mwananchi kufahamu namba yake ya utambulisho kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, kwa waliojisajili itawasaidia kujua hatua ya kitambulisho imefikia wapi.

Ameongeza kuwa huduma hiyo itaondolea wananchi usumbufu na gharama za usafiri kwenda ofisi za NIDA kupata hudua hiyo, kupunguza foleni katika ofisi za mamlaka na itawezesha pia watu kupata hudua ya kufuatilia taarifa zao kwa hatua kila wanapokuwa na uhitaji.

Naye, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, amesima hatua hiyo ni dhamira ya dhati ya NIDA ya kuendana na kasi ya teknolojia katika kurahisisha huduma kwa wananchi, na namba hiyo itamuwezesha mwananchi kufuatilia hatua kwa hatua maombi ya utambulisho wake.

"Itarahisisha huduma za taarifa za mombaji na kuondoa sababu ya kwenda kulundikana katika ofisi za NIDA," amesema.

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: