Mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Hala, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Gabriel Noel (45), amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa kwa kitu kizito na rafiki yake, Adam Keto, katika tukio linalodaiwa kusababishwa na ugomvi wa memory card ya simu.
Tukio hilo limetokea Desemba 17, 2025 katika mazingira ambayo chanzo chake kinaelezwa kuwa ni kugombania memory card hiyo ya simu, kati ya marehemu na mtuhumiwa.
Chanzo; Global Publishers