“Ninawatakia kheri ya Sikukuu ya Krismasi Wakristo na Watanzania wote. Mnaposafiri na kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, tusherehekee kwa furaha na upendo.
Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kutukumbushe upendo kwa
Mwenyezi Mungu, upendo kwa kila mmoja wetu, wajibu wa kujitoa kuwasaidia wenye uhitaji, uvumilivu na unyenyekevu.
Tuendelee kukumbuka wajibu wetu wa kutunza Taifa letu ili lidumu katika amani, utulivu, haki, ukweli na ustawi wa kila mmoja wetu sasa na vizazi vijavyo. Mwenyezi Mungu awabariki nyote.” - Samia
Chanzo; Bongo 5