"Sisi kama viongozi wa dini tunazungumza tunapoona mambo na tuna vyombo vyetu vikubwa ambavyo vina Mamlaka ya kuzungumza.
"Tuna Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), CPCT, TEC na vyombo vingine. Iko Jumuiya ya Maridhiano na amani Tanzania tuna nafasi ya kuzungumza na kuwasihi wanasiasa yake ambayo tunaona sasa hayaendi vizuri.
"Hata wakati wa Ukuta, UKAWA wakati ule imechachamaa wakisema kutakuwa na maandamano ya nchi nzima na hali ilikuwa tete na tishio lilikuwa kubwa. Nakumbuka tulikaa kikao kama viongozi wa dini tuliwaita wagombea wote wa vyama vyote.
"Na tulizozungumza kama viongozi wa dini kwamba madhara yake ni makubwa. Na tunawaambia watu watangulize dini halafu siasa baadae. Msiharibu dini zenu kwa sababu ya siasa. Mambo ya siasa ya kidunia tu.
"Na dini utakwenda nayo hadi akhera ndio itakayokufanya uende peponi au Mbinguni"- Sheikh Dr Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti Wa Jumuiya Ya Maridhiano Na Amani Tanzania-JMAT Na Balozi Wa Amani Duniani Kupitia Shirikisho La Amani Duniani (UPF)
Chanzo: Clouds Media