Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Tabora limefanikiwa kuwaokoa watu wanne, akiwemo mama mjamzito, waliosombwa na maji usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Malolo Manispaa ya Tabora, wakiwa kwenye usafiri wa bajaji wakati mvua kubwa ikinyesha, ambapo abiria wamewahishwa hospitalini, huku dereva wa chombo hicho akidaiwa kutokomea baada ya kuokolewa.
Chanzo; Itv