Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mgombea Ubunge Auwawa na Wananchi Waliojichukulia Sheria Mkononi

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Daudi Wilbard Ntuyehabi ameuawa Wananchi waliojichukulia sheria mikononi usiku wa Oktoba 7 majira ya saa 1:30 katika Kijiji cha Kilingi, Kata ya Sanya Juu, Wilaya ya Siha.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, tukio hilo lilitokana na ugomvi uliotokea kwenye eneo la Baa ambapo Ntuyehabi anadaiwa kumchoma kisu tumboni Abdul Issah Mohamed ambaye ni Mkazi wa eneo hilo aliyekuwa akijaribu kutuliza ugomvi uliotokea kati ya Marehemu na Mtu mwingine walipokuwa wakibishana kuhusu fedha ambapo Abdul Issah Mohamed kwa sasa anaendelea na matibabu hospitalini.

Jeshi la Polisi limesema limewakamata Watu wanane wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo la kujichukulia sheria mkononi akiwemo Hamadi Issah Mohamed, Alphonce Kinyaha, Rizik Amedeus, Frank Paulo Lutindi, Shedrack Emanuel, Jeremia Mnkondo, Zainab Elisha na Issah Mohamed.

Aidha, Jeshi hilo limekemea vikali tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi na limewataka Watu kufuata taratibu za kisheria katika kutatua migogoro ili kuepusha madhara makubwa kama yaliyojitokeza kwenye tukio hilo.

 

Chanzo: Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: