Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mapingamizi ya Saidi Kesi ya Lissu Yakataliwa

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam imeyatupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA Said Issa Mohammed na wenzake wawili ambao ni Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA Zanzibar ambao wanapinga maombi ya Tundu Lissu kukataa kuunganishwa katika Kesi ya mgawanyo wa mali za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Uamuzi huo umetolewa leo Machi 3 2026 na Jaji Hamidu Mwanga baada ya kutupilia mbali mapingamizi hayo yaliyowasilishwa na Wakili wa Walalamikaji, Said Issa Mohammed na wenzake ambapo Mahakama ilieleza kuwa hoja zilizowasilishwa katika pingamizi hilo zinagusa masuala ya ushahidi ambayo hayawezi kuamuliwa katika hatua ya awali ya pingamizi la kisheria.

Katika kesi hiyo ambayo imeahirishwa hadi Machi 6, 2026 kwa ajili ya kusikilizwa, Walalamikaji watatu ambao ni Makamu Mwenyekiti mstaafu Said na wenzake, wanadai kuwa ndani ya Chama hicho kumekuwa na mgawanyo usio sawa wa mali za Chama na rasilimali za kifedha kati ya Zanzibar na Tanzania Bara kinyume na sheria za Vyama vya Siasa na Katiba ya CHADEMA.

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: