Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Malipo ya Kumuona Daktari Yanachukuliwa na Serikali

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Mugisha Nkoronko amesema hakuna ukweli wowote kuwa tozo zinazolipwa na wagonjwa wanapomuona daktari huenda moja kwa moja kwa madaktari, bali ni malipo rasmi ya Serikali kwa ajili ya huduma za matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Dk. Nkoronko amesema hakuna daktari katika hospitali au kituo cha afya cha umma anayepokea fedha hizo mkononi, kwani malipo yote hufanyika kupitia mfumo rasmi wa Serikali kwa kutumia namba za malipo.

Amesema fedha hizo hutumika kuboresha huduma katika hospitali na vituo vya afya, huku akiongeza kuwa kauli zinazoeleza kuwa madaktari hupokea fedha hizo moja kwa moja zinawavunja moyo wataalamu hao na kudhoofisha juhudi zao za kutoa huduma kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Dk. Nkoronko, jukumu la msingi la madaktari ni kuendelea kuwahudumia wananchi na kusaidia kurejesha afya zao, huku akibainisha kuwa daktari bingwa mmoja kwa sasa huhudumia wagonjwa kati ya 35 hadi 40 kwa siku, kiwango alichosema ni kikubwa ukilinganishwa na mataifa mengine.

Aidha, amewataka wanasiasa kuacha kulinganisha taaluma ya udaktari na “bei ya nyanya,” akisisitiza umuhimu wa kuheshimu na kuthamini taaluma hiyo kutokana na gharama kubwa inayotumika kuwaandaa wataalamu wa afya nchini.

Kuhusiana na mada hii: