Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

WAZIRI MASAUNI AIPONGEZA BODI YA WAKURUGENZI NEMC KWA USIMAMIZI WA MAZINGIRA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi NEMC  kwa utekelezaji wa majukumu ya Usimamizi na Uhifadhi wa mazingira.

Waziri  Masauni ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake katika Ofisi za  NEMC jijini Dar es Salaam, ambapo alipokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza.

Amesema taarifa hiyo imeonesha hatua zilizochukuliwa na NEMC katika kusimamia uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira, kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa shughuli zinazoweza kuathiri mazingira, kushughulikia malalamiko ya wananchi na kusimamia taka hatarishi ikiwa ni pamoja na kuongeza uwajibikaji katika kulinda mazingira kwa manufaa ya wananchi na maendeleo endelevu ya Taifa.

Masauni pia amepongeza utekelezaji wa shughuli za kimkakati za Baraza, ikiwemo uzinduzi wa mfumo wa ufuatiliaji wa uchafuzi wa mazingira (TOCEMS), maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Uelimishaji kuhusu Zebaki mkoani Geita, maandalizi ya ujenzi wa ofisi za kudumu Dodoma pamoja na hatua zinazoendelea za kulibadilisha NEMC kuwa Mamlaka ya Taifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA).

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NEMC, Mhandisi Mwanasha Tumbo, amesema Baraza litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uwajibikaji, huku likiimarisha usimamizi wa mazingira na kushirikiana na wadau ili kufikia azma ya maendeleo endelevu ya mazingira.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi, ameeleza kuwa Baraza litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Serikali na wadau katika kuhakikisha mazingira yanalindwa na wananchi wanapata huduma bora.

Katika hatua nyingine, Waziri Masauni  amezindua magari matano kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ukaguzi, ufuatiliaji na upimaji wa mazingira. Magari hayo, yakiwemo Hard Top moja na Prado nne, yatakayoongeza uwezo wa NEMC kufikisha huduma karibu na wananchi, kushughulikia changamoto za kimazingira na kufanya ukaguzi.

Masauni ameitaka Menejimenti kuhakikisha magari hayo yanatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa, yanatunzwa vizuri na kugawanywa kulingana na mahitaji ya maeneo husika.

Kuhusiana na mada hii: