Uhaba wa dawa za kulevya aina ya heroini jijini Tanga umechangia kupungua kwa idadi ya watumiaji, huku baadhi ya waraibu wakilazimika kutumia dawa feki au kukimbilia bangi na pombe.
Matumizi ya dawa za kulevya husababisha madhara makubwa kiafya na kijamii, yakiwemo magonjwa ya akili, maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kupitia matumizi ya sindano zisizo salama, pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na kuvunjika kwa mahusiano ya kifamilia.
Upatikanaji wa dawa za kulevya aina ya heroini umeelezwa kuwa mgumu katika Jiji la Tanga, hali iliyosababisha baadhi ya waraibu kuhangaika kutafuta dawa hiyo, huku wengine wakijiingiza katika matumizi ya heroini feki.
Mratibu wa Gift of Hope, Said Bandawe, amesema matumizi makubwa ya dawa za kulevya yalikuwa ni heroini huku Afisa kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Shaban Miraji, akizungumzia kuhusu uanzishwaji wa vituo vya Methadone vinavyolenga kutoa huduma kwa waraibu wa dawa za kulevya.
Mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya serikali, wataalamu wa afya na jamii kwa ujumla, ili kuokoa nguvu kazi ya taifa na kulinda kizazi cha sasa na kijacho dhidi ya janga hio.
Chanzo; Clouds Media