Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwigulu Kivukoni Vigogo TAMESA Wang’olewa

Waziri Mkuu, Dkt. Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza kufutwa kazi na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) pamoja na menejimenti ya wakala huo kutokana na ubadhilifu wa zaidi ya shilingi bilioni 2.5.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega kufanya uchunguzi wa vivuko vyote ili kubaini vyanzo vya uharibifu kwa sababu kuna taarifa kwamba vivuko hivyo vinaharibiwa kwa makusudi ili wahusika waweze kujipatia fedha kupitia matengenezo.

Amesema uamuzi huo unatokana na matokeo ya tume maalumu iliyoundwa ndani ya kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma katika wakala huo.

“Vyombo husika vichukue hatua kwa wahusika, haya mambo ya kutoheshimu fedha za umma, kutokuwa na huruma na Watanzania lazima yafike mwisho.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Jumatano, Desemba 24, 2025 akizungumza na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam na wakazi wa Kigamboni akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji wa huduma katika kivuko cha Magogoni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Amesema ubadhilifu uliofanyika ni sawa na watendaji hao kugawana vivuko pamoja na kuiba nauli zinazotolewa na wananchi mambo ambayo yanamkera Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na amewaagiza wayakomeshe ili wananchi waendelee kupata huduma bora na za uhakika.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega afanye mawasiliano na wizara ya fedha kuhakikisha fedha za malipo ya utengenezaji wa vivuko zinatolewa kwa wakati ili zoezi la ukarabati liweze kukamilika na vivuko hivyo viweze kutoa huduma.

Serikali inavivuko vitatu katika eneo la Kivukoni/Kigamboni na kwa sasa kinachonfanyakazi ni kimoja tu.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Moses Mabamba amesema Serikali inamiliki vivuko vitatu kwa ajili ya Kivukoni na Kigamboni ambapo kwa sasa kinachotoa huduma ni kimoja tu cha MV.

Kazi huku kivuko cha MV. Magogoni kipo kwenye matengenezo Mombasa tangu 2023.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: