Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na Said Issa Mohammed na wenzake kupinga Lissu kuunganishwa katika Kesi ya Mgawanyo wa Mali inayowakabili Katibu Mkuu wa CHADEMA na Bodi ya Wadhamini.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Hamidu Mwanga, baada ya kutupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na Wakili wa walalamikaji (Said Issa Mohammed na Wenzake), na kwa msingi huo maombi ya msingi ya Lissu yatasikilizwa Machi 06, 2026 mbele ya Jaji Hamidu Mwanga.
Chanzo; Nipashe