Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA, John Mnyika amesema amepata taarifa kutoka kwa mmoja wa kiongozi wa Jeshi la Polisi kwamba Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche yupo Dodoma.
Akizungumza nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam, Mnyika amesema;
“Tunalitaka Jeshi la Polisi na Uhamiaji kwa pamoja watoe kauli kwa umma kwamba Makamu Mwenyekiti John Heche yupo wapi na ana hali gani, Makamu Mwenyekiti alichukuliwa asubuhi kweupe mbele ya mahakama na alichukuliwa na Polisi, kwa wenye wajibu wa kusema yupo wapi ni na ana hali gani wa kwanza kabisa ni Jeshi la Polisi na wapili ni idara ya uhamiaji, kwa nafasi yangu nimefanya mawasiliano na kiongozi mmoja wa Jeshi la Polisi akanieleza kwamba Makamu Mwenyekiti yupo Dodoma na akasema tufuatilie Dodoma,
Chanzo: Millard Ayo