kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna Wilbrod Mutafungwa amesema tarehe 24 mwezi wa pili mwaka huu katika mtaa wa Bushata kisiwa cha Bezi majira ya saa mbili usiku mvuvi aitwaye Aboubakar Shaban Ramadhan (44) alizama ziwani na kupoteza maisha wakati akiendelea na shughuli zake za uvuvi
Tukio la pili limetokea Machi 1, 2026 majira ya saa 2:00 asubuhi katika Mtaa wa Mtakuja, Kata ya Nyamhongolo, Wilaya ya Ilemela, ambapo ulipatikana mwili wa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 hadi 50.
Kamanda Mutafungwa amesema mwili huo ulikutwa katika shamba la miwa lililopo kwenye bonde la Mto Maji ya Rangi na uchunguzi wa awali unaonesha huenda marehemu alisombwa na maji kutoka eneo jingine kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kushindwa kuhimili nguvu ya maji.
Chanzo; Clouds Media