Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Makamu Mwenyekiti Taifa, John Heche anashikiliwa kwenye mahabusu ya jeshi la Polisi Mtumba jijini Dodoma lakini amenyimwa dhamana.
Katika taarifa iliyotolewa na chama hicho kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa licha ya mawakili wa chama hicho kufika kumpa msaada wa kisheria lakini walinyimwa kumuwekea dhamana.
Heche alikamatwa na Jeshi la Polisi siku ya Jumatano kwenye lango la kuingilia Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es salaam kisha kusema wanampeleka mkoani Mara hata hivyo mawakili na ndugu wa kiongozi huyo walipomfuatilia katika vituo vya polisi mkoani Mara hawakufanikiwa kumuona.
Chanzo: Nipashe