Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Dk.Charles Kitima ameeleza jinsi alivyo na hofu ya kushambuliwa tena na watu wasiojulikana baada ya tukio baya la kushambuliwa miezi kadhaa iliyopita akiwa katika makazi ya maaskofu Kurasini jijini Dar es Salaam.
Padri Kitima aliyasema hayo jana wakati akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu mpya wa baraza hilo Padri Dk. Faustine Furaha wa Jimbo Katoliki Moshi ambaye amechukua nafasi ya Padri Chesco Msaga aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Kristo Duniani.
Padri Kitima alieleza ambavyo alilazimika kumtuma Padri Chesco Msaga mahali ambapo yeye aliogopa kwenda kutokana na hofu ya kushambuliwa tena na watu wasiojulikana.
"Mimi sasa hivi naishi kwa hofu sana lakini yeye (Padri Chesco Msaga) hana hofu mimi naishi kwa hofu natafutwa sijui niuawe, sijui kitu gani, lakini 'father' yeye ana amani kabisa namtuma hebu nenda mjini ujue mimi natufutwa nisije nikatekwa"-Padri Charles Kitima
Chanzo; Nipashe