Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Necta Yatangaza Matokeo ya Darasa la Saba

Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika kuanzia Septemba 10, 2025.

Matokeo hayo yametangazwa leo, Jumatano Novemba 5, 2023 na Katibu Mtendaji wa Necta, Profesa Said Ally Mohamed.

Jumla ya watahiniwa 1,172,279 walifanya mtihani huo kati ya hao wavulana ni 535,138 sawa na asilimia 45.65 na wasichana ni 637,141 sawa na asilimia 54.35.

Ufaulu wa jumla wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2025 umeongezeka kwa asilimia 0.93, ambapo jumla ya watahiniwa 937,581 sawa na asilimia 81.80 kati ya 1,146,164 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B na C.

Takwimu hizo zimetolewa leo na Necta, zikionesha ongezeko la ufaulu ukilinganisha na mwaka 2024 ambapo watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 80.87.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kati ya waliofaulu, wavulana ni 429,104 sawa na asilimia 82.51, huku wasichana wakiwa 508,477 sawa na asilimia 81.21.

Aidha, Necta imeeleza kuwa ubora wa ufaulu nao umeimarika, ambapo jumla ya watahiniwa 422,923 sawa na asilimia 36.90 wamepata madaraja ya juu (A na B), ikilinganishwa na asilimia 35.83 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 1.07.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: