Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Dada na Kaka Jela Kwa Kujamiana, Wakana Sio Ndugu

Mahakama ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela Kijana aitwae Musa Shija (32) na kifungo cha miaka 30 jela Bi. Hollo Shija (36) kwa kosa la kujamiana hadi kupata Mtoto wakati wao ni Ndugu wa damu waliotokana na Baba mmoja na Mama mmoja.

Hukumu hiyo imesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Aziz kwa Washtakiwa hao ambao ni Wakulima Wakazi wa Kijiji cha Mandang’ombe baada ya Mahakama kujiridhisha pasi na shaka kupitia vielelezo ikiwemo vipimo vya DNA na Mashahidi 11 waliothibitisha makosa hayo.

Hakimu amesema kosa la Ndugu kujamiiana ni kinyume na kifungu cha 158 cha kwanza (b) na kifungu cha 160 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 6 marejeo ya mwaka 2022 ambapo kwa mujibu wa maelezo ya upande wa mashtaka ukiongozwa na Mkaguzi wa Polisi Vedastus Wajanga kati ya mwaka 2018 hadi July 30,2024 Washtakiwa walikuwa wakiishi pamoja kama Mume na Mke na wakapata Mtoto mmoja.

Washtakiwa walifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza August 12,2025 ambapo walikiri makosa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa Mussa na 30 kwa Horro kisha wakakata rufaa Mahakama Kuu na ikaamuru kesi isikilizwe upya ambapo kesi ilianza upya Mahakama ya Maswa na May 06,2025 walifikishwa Mahakamani na kusomewa mashtka yao na wakakana kutenda licha ya vipimo vya DNA kuonesha Mtoto wao ana uhusiano nao wa damu 99.9%.

Katika utetezi wao Mussa alidai yeye ni hatma na Horro ni Mke wake halali ambaye alimtolea mahari ya Tsh. laki 3 na elfu 25 kwa Bibi yake na Horro amedai Mussa ni Mumewe na wote wawili wamekanusha kuwa Mzee Shija Kamuga sio Baba yao Mzazi bali ni jirani mwenye chuki dhidi ya ndoa yao lakini pamoja na utetezi wao Hakimu akawahukumu kwenda jela.

 

Chanzo: Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: