Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mzozo wa Iran Mafuta Bei Yapaa

“Kama tunavyoona misukosuko iliyotokea hapa karibuni wiki iliyopita na tunayoendelea nayo, tayari imeshapandisha bei ya mafuta kwa 13% hadi jana, sasa hatujui leo na siku zijazo lakini tumuombe Mungu watu wale wakae juu ya meza wazungumze wakubaliane na misukosuko hii iishe ili dunia irudi katika hali ya kawaida kuendesha chumi za Nchi zetu, ni vema kutokana na mabadiliko hayo ya dunia kukawa na mradi ili kujihakikishia usalama wa mafuta”

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema misukosuko iliyotokea hivi karibuni baada ya uwepo wa mapigano kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran tayari imepeleka bei ya mafuta duniani kupanda kwa 13% hadi jana ambapo amesema kutokana na misukosuko ya aina hiyo Tanzania ina kila sababu ya kuimarisha akiba ya kimkakati ya hifadhi ya mafuta ili hata bei ikipanda Tanzania isiathirike.

Rais Samia amesema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Matanki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es salaam katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es salaam, leo March 03, 2026.

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: