Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Pombe Magufuli, Bi. Suzana Musa ameagwa rasmi leo Mei 29, 2026 katika Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita. Bi.
Suzana aliyefariki dunia Mei 25, 2026 ameagwa na mamia ya Waombolezaji wakiwemo Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Baada ya ibada ya kuaga, Bi.Suzana amezikwa katika Makaburi ya familia yaliyopo Chato.