Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Utata Kifo cha Irene Wawaibua The Hub

Sakata la kifo cha Irene Mallya, mwenye umri wa miaka 24, mkazi wa Mtaa wa Lemara, Kata ya Lemara jijini Arusha, limeibua maswali mbalimbali baada ya mwanamke huyo kufariki dunia kufuatia kudaiwa kujeruhiwa kwa chupa akiwa pamoja na wenzake katika eneo la burudani jijini humo.

Baada ya tukio hilo, jina la eneo la burudani la 'The Hub', lililopo jijini Arusha, lilianza kutajwa katika mijadala mbalimbali kuhusiana na tukio hilo.

Kutokana na hilo, mwandishi wa Global TV mkoani Arusha, Korumba Lebabaz, alimtafuta Mkurugenzi wa The Hub ili kupata ufafanuzi kuhusu madai ya eneo hilo kuhusika na tukio lililosababisha kifo cha Irene.

Akizungumza na Global TV, Mkurugenzi huyo ameeleza kilichobainika kupitia kamera za CCTV zilizokuwa zikirekodi matukio katika eneo hilo, akisema picha hizo zinaonyesha Irene akiondoka katika eneo la The Hub akiwa salama.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, hakuna tukio lililonaswa na kamera hizo linalomuonyesha Irene akijeruhiwa au kukumbwa na tukio lolote ndani ya eneo la The Hub ambalo linaweza kuhusishwa moja kwa moja na kifo chake.

Kuhusiana na mada hii: