Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ubunifu wa Tanzania Wavuka Mipaka

Chuo cha Maji (WI) kimepokea ujumbe kutoka Ghana Water Limited na Ghana Water Institute, waliokuja Tanzania kujifunza kuhusu teknolojia ya Integrated Leakage Management System (ILMS) iliyobuniwa na Chuo cha Maji.

ILMS inasaidia mamlaka za maji kufuatilia na kupunguza upotevu wa maji, kuboresha uendeshaji na kukabiliana na changamoto ya Maji Yasiyo na Mapato (NRW) kwa kutumia teknolojia na takwimu.

Mkuu wa Chuo cha Maji, Prof. Adam O. Karia, amesema ziara hiyo ni ishara nzuri kwamba ubunifu unaofanyika Tanzania unaweza kuvuka mipaka na kusaidia kutatua changamoto za maji katika nchi nyingine.

Kiongozi wa Mradi, Eng. Dr. Ghanima Chanzi, amesema hamasa kutoka Ghana inaonesha uwezo wa suluhisho zinazobuniwa Afrika katika kutatua changamoto za Afrika.

Ni hatua ya kujivunia kwa Chuo cha Maji na Tanzania kwa ujumla katika kukuza ubunifu na uhawilishaji wa teknolojia barani Afrika. 

Kuhusiana na mada hii: