Serikali imeanza mpango wa kukiunganisha Kitambulisho cha Taifa (Nida) na huduma nyingine za umma ikiwamo bima ya afya, leseni ya udereva na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuepusha utitiri wa vitambulisho pindi mtu anapohitaji huduma mbalimbali.
Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameeleza hayo, leo Ijumaa Desemba 19, 2025 katika kikao kazi cha tathimini ya utekelezaji wa ahadi za siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho kilichofanyika wilayani Kibaha mkoani Pwani, kimehudhuriwa na mkuu wa mkoa huo, Abubakari Kunenge, wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa juu wa ngazi ya mkoa huo.
Chanzo; Mwananchi