Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mvua Kubwa Kuchapa Mikoa 20 Tanzania

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa 20 nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA, leo Jumamosi Desemba 27, 2025 imetaja mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Morogoro, Ruvuma, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia.

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha Jumapili, Desemba 28, 2025, na huenda zikasababisha madhara mbalimbali ikiwamo mafuriko, maporomoko ya udongo na usumbufu wa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyotajwa, hususan walioko mabondeni na maeneo hatarishi, wametakiwa kuchukua tahadhari za mapema ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

TMA imewasisitiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa na utabiri wa hali ya hewa unaotolewa mara kwa mara ili kupata taarifa sahihi na za wakati.

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: