Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Helkopta Yaanguka na Kuua Watano Mlima Kilimanjaro

Helkopta ya kampuni ya uokoaji ya KiliMediaur Aviation imepata ajali maeneo ya kati ya Kibo na Barafu Camp katika Mlima Kilimanjaro na kusababisha vifo vya watu watano.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, leo Desemba 24, saa 11:30 ikiwa inatoka kuchukua wagonjwa wa kampuni ya Utalii
Boby Camping.

“Ni kweli kuna ajali ya helkopta ya kampuni ya uokoaji ya
KiliMediar na waliofariki ni wageni wawili, guide (muongoza watalii) mmoja, rubani na daktari, taarifa zaidi zitapatikana kesho asubuhi,” amesema kamanda Maigwa.

Taarifa kutoka eneo la tukio ambazo bado hazijathibitishwa zinaeleza kuwa baada ya helikopta hiyo kuanguka ililipuka moto na kusambaratıka huku jitihada za uokoaji zikifanyika.

Eneo la Kibo Hut na Barafu Camp ni urefu wa kati ya mita
4,670 na meta 4,700 kutoka usawa wa bahari.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: