Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, John Heche amekamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi muda mfupi baada ya kuwasili Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam.
Camera za Ayo Tv zimenasa tukio hilo ambapo Askari Polisi waliingia katika gari ambalo ndani yake alikuwepo Heche na kisha kuondoka naye.
Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema hawajafahamishwa sababu za kukamatwa kwa Heche.
Chanzo: Millard Ayo