Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watoto Chini ya 18 Kupewa Namba ya Utambulisho

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa George Simbachawene, amesema Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inaendelea na maandalizi ya kuanza usajili wa watoto walio chini ya umri wa miaka 18, kwa lengo la kuwapatia namba ya utambulisho ya kipekee itakayomfuata mtu tangu kuzaliwa hadi mwisho wa maisha yake.

Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa Agosti 10, 2023.

Mheshimiwa Simbachawene ameyasema hayo baada ya kutembelea Kituo cha Uchakataji Taarifa cha NIDA, ambako alijionea shughuli za uzalishaji wa vitambulisho vya taifa zinavyoendelea. Aidha, wilaya tatu zimechaguliwa kuanza zoezi hilo la usajili, ambazo ni Kilolo, Kusini Unguja na Rungwe.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Omar Mmanga, ametoa maelezo kuhusu hatua iliyofikiwa katika usajili wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: