"Viongozi wa chama kupitia kwa Mkurugenzi wa chama Gaston Garubindi ambaye ni wakili na Mkurugenzi wa masuala ya sheria wa CHADEMA wamefika 'Central' polisi kumuulizia mheshimiwa John Heche wakaambiwa ni kweli amefika hapa lakini tunamsafirisha kwenda Tarime"
"Sasa katika hali ya kutushangaza mtu ambaye ni kiongozi ambaye anaweza kuitwa polisi kwa barua au kwa meseji na akaenda wamechukua jukumu la kumbeba kutoka Dar es Salaam na kumsafirisha"
"Umbali wa kutoka Dar es Salaam mpaka Tarime hata kama umesafiri kwa basi jana saa saba usiku leo unakuwa umeshafika lakini pia kama ni pikipiki kwa muda wote huo ingekuwa imeshaingia pia"-Chacha Heche
Chanzo: Nipashe