Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

14 Wanusurika Kifo Morogoro

Watu 14 wakiwemo Wanaume 11 na Wanawake watatu wamenusurika kifo kufuatia ajali ya basi na Lori ilililotokea asubuhi ya leo Desemba 24, 2025 katika eneo la Magubike, Kata ya Magubike, Wilaya ya Kilosa barabara ya Morogoro-Dodoma huku chanzo cha ajali hiyo kilitajwa na uzembe wa dereva wa basi

Akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema ajali hiyo imesababisha majeruhi kwa watu kumi na nne, ikihusisha magari mawili yaliyogongana uso kwa uso gari la kwanza ni basi lenye namba za usajili T 577 DXL, mali ya Kampuni ya NASRI – Yutong, likiendeshwa na dereva Alex Patric (40), mkazi wa Milandizi, Pwani, likitokea Tarime kuelekea Dar es Salaam.
Gari la pili ni lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 145 AFA / T 148 AFK, mali ya Kampuni ya ATT, likiendeshwa na dereva Robert Manunu (30), mkazi wa Bariadi, likitokea Morogoro kuelekea Tabora.

Majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa katika Kituo cha Afya Magubike kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kamanda Mkama amesema Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi aliyetaka kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari, hali iliyosababisha ajali hiyo ambapo Dereva huyo wa basi anapatiwa matibabu chini ya Ulinzi Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: