Mtu mmoja ambaye ni Mwanaume ameondolewa ndani ya chumba cha Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ndogo ya Dar es salaam baada ya kupiga kelele akiwa ndani ya Chumba cha Mahakama baada ya Majaji kuingia.
Tukio hilo lilitokea wakati Watu wote ndani ya ukumbi wa Mahakama wakiwa wametulia tayari kwa kesi inayoendelea dhidi ya Tundu Lissu ambapo mbele ya Jopo la Majaji watatu likiongozwana Jaji Dastan Ndunguru, Jaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde Mwanaume huyo alianza kuongea kwa sauti kubwa.
Sauti yake ilisikika kutoka ukumbi wa juu wa Mahakama ikisema maneno yafuatayo “Waheshimiwa Majaji wa Mahakama hii naomba mnisilikiize nimetumwa na Mungu” ambapo Askari waliwahi kumfikia na kumbeba kumtoa nje ya ukumbi Mahakama huku akisikika akisema “Yesu Nitetee, Yesu ndio Mwokozi wangu”
Chanzo: Millard Ayo