Baraza maalum la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo lilioketi December 22, 2025 likiongozwa na Mstahiki Meya Lawrence Mlaki limewachukulia hatua Watumishi watano kwa mashauri mbalimbali ya kinidhamu
Watumishi hao ni pamoja na Mtendaji wa Kata, aliyekuwa anatuhumiwa kwa makosa ya utoro kazini, Muuguzi ( Mtaalam wa dawa ya usingizi) aliyeshindwa kutekeleza ipasavyo majukumu aliyopangiwa na Mwajiri.
Wengine ni Muuguzi Mkuu, Mteknolojia Mkuu na Mteknolojia Msaidizi Mwandamizi Mkuu ambao walikutwa na kosa la vyeti feki( walioguhushi vyeti).
Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo ya masuala ya kiutumishi, Baraza limeridhia kuwafukuza kazi Watumishi watatu walioghushi vyeti pia likiridhia kurudishwa kazini Mtumishi aliyetuhumiwa kwa utoro kazini na kushauri asipewe adhabu yoyote baada ya kukutwa hana hatia
Baraza limeelekeza Mtuhumiwa aliyempatia Mgonjwa huduma chini ya kiwango ikiwa ni pamoja ya kutompeleka wodini, kukatwa asilimia 15 ya mshahara wake kwa kipindi cha miaka 3.
Chanzo; Millard Ayo