Mgombea Ubunge kupitia Jimbo na Pangawe Omar Said Shaaban amezitaja kasoro ambazo kwa upande wake amezishuhudia akiwa kwenye Kituo chake cha Kupiga Kura cha Pangawe ikiwemo kuwepo kwa idadi kubwa ya wapiga kura ambap ni Wanajeshi na wengine ambao wamevalia nguo za Jeshi ambazo kwenye upande wa kifua zikiwa hazina majina (Name Tag) jambo ambalo ameliona ni hujma
Omar ameyasema hayo akiwa kwenye kituo cha Pangwe ikiwa leo hii Zanzibar imeanza kura ya mapema inayowahusu watu maalum ambapo ameshudua kasoro nyengine ikiwemo wapiga kura kuchovya wino kidogo na baadhi ya vitu muhimu kutotolewa vikiwa ni vitendea kazi
Nae Mgombea Uwakilishi Jimbo la Mji Mkongwe nae amewaangushia lawama tume ya uchaguzi kwa kile alichodai kua idadi ya watu imeonekanw kuongezeka tofauti na ya awali ambapo amedai kua kumekua na watu ambao wamekua wanarudia rudia zoezi hilo
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar Jaji George Kazi amesema kulikua na Changamoto kwa Kituo cha Pangawe lakini waliwasiliana na Mgombea Ubunge Act Omar Shaaban na kutatua changamoto hizo ,akifafanua ishu ya wanajeshi walioonekana kua wengi katika kituo hicho amesema wote waliopiga kura walistahiki kwani wali ni wananchi na wameandikishwa na kuombewa
Chanzo; Millard Ayo