Baada ya kusambaa mitandaoni kwa taarifa za Mfanyabiashara Jenifer Jovin ( Niffer) kutekwa na Watu wasiojulikana leo Dukani kwake maeneo ya Sinza Kumekucha Jijini Dar es salaam, Ayo Tv imelitafuta Jeshi la Polisi ili kufahamu kuhusu tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro ameithibitishia Ayo Tv kuwa Jeshi la Polisi ndilo lililohusika kumkamata Mfanyabiashara huyo huku akisisitiza yafuatayo, Polisi wamemkamata wala sio Watu, sema Polisi wamemkamata mi ndio nakwambia” amesisitiza Kamanda Muliro.
Chanzo: Millard Ayo