Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Lissu Aomba Dhamana, Mahakama Yatupulia Kapuni

Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imelikataa ombi la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu la kutaka apewe dhamana. Lissu aliwasilisha hoja hiyo leo Ijumaa, Oktoba 24, 2025 baada ya Jamhuri kuomba kesi iahirishwe kutokana na kutokuwa na shahidi kwa siku ya leo.

Awali, Jamhuri katika kesi hiyo ya uhaini inayomkabili Lissu, iliomba iahirishwe mpaka Novemba 3, 2025 kwa kuwa leo hawana shahidi.

Kesi hiyo inayosikilizwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Iringa, Dunstan Ndunguru akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde ilitarajiwa kuendelea kusikilizwa leo Oktoba 24, 2025.

Hata hivyo, Jamhuri imeieleza Mahakama kuwa kwa leo hawana shahidi kwa kuwa mashahidi waliokuwa wanafuata kutoa ushahidi wao unahusiana na vielelezo vilivyokataliwa Oktoba 22 na 23, 2025.

Vielelezo hivyo ni vihifadhi data (flash disk na memory card) zenye picha mjongeo yenye hotuba ya Lissu yenye maudhui yanayodaiwa kuwa na maneno ya kuitishia Serikali ambalo ni kosa la uhaini.

 

Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: