Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema hawajapokea taarifa yoyote kutoka kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Dkt. Charles Kitima juu ya madai ya kutaka kuuliwa.
Akijibu swali la Mwandishi wa AyoTV leo Kamanda Muliro alisema “Ndio nimesikia kutoka kwako, kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda kila Mtu wakiwemo Ma-Father”.
Itakumbukwa hivi karibuni, Padri Kitima alisikika akizungumzia hofu ya maisha yake wakati akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu mpya wa Baraza hilo Padri Dkt. Faustine Furaha wa Jimbo Katoliki Moshi ambaye amechukua nafasi ya Padri Chesco Msaga aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Kristo Duniani.
Chanzo; Millard Ayo