Baada ya taarifa kuzaga ndani ya mitandao ya kijamii zikimuulizia mwanamitandao maarufu Clemence Mwandambo Jeshi la Polisi lasafisha anga hilo.
Ambapo taarifa zinasema, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Awali ya "Saint Clemence" ndugu Clemence Kenani Mwandambo, mkazi wa Uzunguni "A". Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashifu imani za dini zingine.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo Disemba 29, 2025 saa 4:00 asubuhi maeneo ya Uzunguni. Jijini Mbeya akichapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashifu imani ya dini ya kiislamu na kikristo kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Upelelezi unakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Chanzo: Tanzania Journal