Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio la ukatili dhidi ya mtoto wa miaka 10 katika Wilaya ya Urambo, Mkoa wa Tabora, lililofanyika Machi 2, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, picha zilizosambaa mitandaoni zikimuonesha mtoto akifungwa kamba miguu na mikono kisha kuning’inizwa dirishani zinahusiana na tukio hilo. Mtoto huyo alipelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kuokolewa.
Mtuhumiwa wa tukio hilo ametajwa kuwa Joseph Mbalamwezi Fransis, mkazi wa Imalamakoye B, Urambo, ambaye ni mjomba wa mtoto huyo. Inadaiwa alimchukulia hatua hiyo baada ya mtoto kuangusha nyama aliyokuwa anapika.
Polisi mkoani Tabora wamemkamata mtuhumiwa na wanaendelea na hatua za kisheria.
Chanzo; Itv