Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ruwa’ichi na Ugomvi na Mtu Anayepigania Haki

'Sina ugomvi na mtu yeyote anayepigania amani.
Lakini nikuambia kwamba, kwa hakika, huwezi kuwa na amani bila haki.
Amani na haki ni vitu viwili vinavyotegemezana.''

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Tanzania, Mhashamu sana Juda Thaddeus Ruwa'ichi, amesema Watanzania wengi hawashabikii haki wala siyo wadau wa haki. Askofu Ruwa'ichi aliyasema hayo katika misa ya mkesha wa Krismasi jijini humo.

"Ewe Mtanzania kama utaka kujigamba kuwa mtu wa amani, jitose kupigania haki, jitose kusema kweli, amani na mambo yanayompendeza Mungu,"

Kumekuwa na mgawanyiko baina ya viongozi hususan wa dini wanaosisitiza sharti kuwe na amani na wale wenye wanaosisitiza kupigania haki ya watanzania kabla na baada ya vitendo vya uvunjifu wa amani, vurugu, machafuko na mauaji yaliyotokea siku na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 nchini Tanzania.

 

 

Chanzo; Bbc

Kuhusiana na mada hii: