Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Musa Apoteza Maisha Baada ya Mtungi wa Gesi Kulipuka

Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kupigwa kipande cha mtungi wa gesi uliolipuka katika eneo la Masiwa, Kata ya Dunda, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Tukio hilo lilitokea leo Jumamosi Oktoba 18, 2025 saa 11:30 wakati kijana mmoja, Musa Rashid (19), mkazi wa Masiwa, anayejihusisha na ukusanyaji wa vyuma chakavu, alipokuwa akigonga kifuniko cha mtungi wa gesi aina ya Carbon dioxide wenye uzito wa kilo 20 kwa kutumia nyundo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salon Morcase, aliyoitoa leo, mlipuko huo ulitokea baada ya kifuniko cha mtungi huo kulipuka kwa kasi na kumgonga kichwani Mengi Waziri (25), mkazi wa eneo hilo, aliyekuwa umbali wa takribani mita 10 kutoka eneo la tukio na kusababishia kifo chake, papo hapo.

Mwili wa marehemu Waziri umehifadhiwa katika Hospitali ya Bagamoyo kusubiri taratibu za uchunguzi na mazishi.

Kamanda huyo ametoa tahadhari kwa wananchi, hasa wanaojihusisha na biashara ya vyuma chakavu, kuacha tabia ya kugonga au kukata vifaa visivyojulikana ambavyo vinaweza kuwa na gesi au mabaki ya kemikali hatarishi, kwani vinaweza kusababisha milipuko na madhara makubwa.

 

 

Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: