Kupitia mtandao wake wa X, David Kafulila, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi Tanzania (PPP Centre), ameandika:
Uamuzi wa kuongeza posho ya kujikimu (boom) kwa wanafunzi wanaopata mkopo kutoka shilingi 8,500 iliyodumu kwa miaka mingi na kuiongeza kufikia shilingi 10,000 kwa siku, ni kwa ajili ya kusaidia watoto wa familia masikini kuweza kumudu gharama za maisha wakiwa chuoni.
Chanzo; Global Publishers