Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Jela Miaka 40 kwa Kuzini na Ndugu

Yaledi Sinkala (38), mkazi wa wilaya ya Momba, mkoani Songwe, amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuzini na maharimu (ndugu) wake mwenye changamoto ya afya ya akili.

Hayo yamebainishwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augostino Senga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya jeshi hilo katika kudhibiti matukio ya uhalifu , pamoja na namna jeshi hilo lilivyojipanga kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kamanda Senga alisema mtuhumiwa huyo baada ya kukamatwa na jeshi hilo na kufikishwa katika mahakama ya Wilaya hiyo, Novemba 18, 2025 alikutwa na hatia na kufungwa miaka 40.

Aidha, Kamanda Senga alibainisha kuwa kupitia oparesheni na mikakati hiyo ya kudhibiti uhalifu, Jeshi hilo limefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wengine wawili kwa makosa mbalimbali, ambao pia wamehukumiwa vifungo vya muda mrefu.

 

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: