Katika muendelezo wa operesheni dhidi ya dawa za kulevya, Jashi la Polisi mkoani Morogoro, limewakamata watu 100 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya dawa hizo. Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP Andrew Kantimbo, akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari mkoani humo, amesema watu 99 wamekamatwa kwa kujihusisha na utumiaji na usafirishaji wa bangi, ambapo walikamatwa wakiwa na Kilograms 118 na gramm 900 za bhangi na bunda 83 za mirungi.
Amesema katika operesheni hiyo, mtu mmoja alikamatwa akiwa anasafirisha viroba viwili vya bhangi vyenye uzito wa Kg 35 kwenye gari aina ya Nissan Patrol yenye namba za usajili DFP 6511. Katika tukio jingine, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kupatikana na nyara za serikali bila kibali, ambapo wamekutwa na vipande 34 vya nyama za swala na Nyati, huku watu wengine 39 wakikamatwa kwa tuhuma za kuuza pombe aina ya gongo kwenye vilabu bubu vya pombe pembezoni mwa Mji Manispaa ya Morogoro.