Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Tanzania Yatoa Wito wa Amani Gaza

Tanzania imetoa wito wa kulindwa kwa raia, kuruhusiwa kwa msaada wa kibinadamu bila vikwazo na kuhuishwa kwa diplomasia yenye lengo la kupata amani ya kudumu katika ukanda wa Gaza na Mashariki ya Kati.

Akihutubia Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 22, 2026, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema Tanzania inaendelea kusisitiza umuhimu wa kupatikana kwa suluhisho la kudumu kwa mgogoro wa Israel na Palestina.

Ndejembi ameongeza kwa kusema kuwa, Tanzania inaunga mkono suluhisho la nchi mbili, ambapo Israel na Palestina zitaishi pamoja kwa amani na usalama, kwa kuzingatia sheria za kimataifa na maazimio husika ya Umoja wa Mataifa.

Vilevile amesema Tanzania inatambua haki ya watu wa Palestina ya kujitawala na kwamba amani ya kudumu inapaswa kuzingatia utu, usalama na matarajio halali ya pande zote mbili.

"Msimamo huo umekuwa sehemu ya sera ya Tanzania ya mambo ya nje kwa miongo kadhaa." " Amesema Ndejembi

Kuhusiana na mada hii: